Habari
Viongozi mikoa, wilaya watakiwa kusimamia usafi
Serikali inatoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa kwa kuzingatia maslahi ya makundi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameyasema hayo mara baada ya kuongoza zoezi la usafi katika Soko la Buguruni Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026.
“Tunakumbuka kuwa Serikali kupitia Mheshimiwa Rais akiwa Makamu wa Rais mwaka 2016 alitoa agizo kuwa kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi kuwa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa.
Aidha Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa ‘Enviromental Management (Designation of National Cleanliness Day) Guidelines , 2016,chini ya G.N.No.139. Mwongozo huo unaelekeza utekelezaji wa tamko la Serikali la kuitangaza kila jumamosi ya mwisho wa Mwezi kuwa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa.
“Kwa muktadha huo, Serikali inatoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa maelekezo haya kwa kuzingatia maslahi ya makundi mbalimbali.



