SADC wampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushindi katika Uchaguzi Mkuu

Nov, 08 2025

Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushindi aliyoupata katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao

Mkutano huo umeridhia nchi ya Afrika Kusini kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mpito mpaka kufikia mwezi Agosti 2026.

Mkutano huo umekubaliana kuendelea kutumia kauli mbiu ya Mkutano wa 45 wa SADC uliyofanyika nchini Madagascar ambayo ni “Kuimarisha Viwanda, Mapinduzi ya Kilimo, Mabadiliko ya Nishati kwa SADC yenye Uhimilivu”

Mkutano huo umeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa na kuhudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na Wawakilishi kutoka Nchi 15 za SADC.

Settings