Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Ndejembi azitaka wizara kuongeza kasi ya kuwaunganishia vijana fursa za maendeleo

Oct, 14 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameonesha kutoridhishwa na kasi ya kuunganisha mifumo inayobuniwa na Taasisi na Wizara zinazoshughulika na masuala ya vijana katika kuwawezesha kupata fursa za maendeleo.

Mhe. Ndejembi amezitaka Wizara na Taasisi hizo kuongeza juhudi, kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha mifumo inayobuniwa inaleta matokeo yenye tija kwa vijana, badala ya kuishia kwenye usajili na ukusanyaji wa taarifa pekee.

Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo alipotembelea Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika sambamba na kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mkoani Rukwa.

Akiwa katika Banda la Ofisi ya Rais - Vijana, Makamu wa Rais alipata maelezo kuhusu Mfumo wa Usajili wa Vijana (YES), ambao hadi sasa umesajili vijana 22,572 na kuwa na fursa 7 pekee.

Baada ya kupokea maelezo hayo, Makamu wa Rais amezitaka Wizara ya Vijana na Wizara ya inayoshughulikia masuala ya Kazi na Ajira, kuunganisha mifumo inayowalenga vijana ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kuongeza uwezo wa Serikali kuwaunganisha vijana na fursa halisi za maendeleo.

Amesisitiza kuwa Serikali ni moja, hivyo taasisi zake zinapaswa kuzungumza lugha moja na kujenga mifumo inayokamilishana, badala ya kufanya kazi kwa kujitenga.

Makamu wa Rais amesema jitihada za kuwawezesha vijana zinapaswa kupimwa kwa matokeo yanayoonekana katika maisha yao, si kwa idadi ya vijana waliosajiliwa kwenye mifumo pekee.

Amesema bado kuna kazi kubwa ya kuhakikisha vijana wanafikiwa na fursa za kiuchumi na kijamii, na kwamba mifumo inayobuniwa na Serikali lazima iwe nyenzo ya kutatua changamoto zao na kuwaunganisha na fursa zinazoweza kubadilisha maisha yao.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka watendaji kutoka maofisini na kwenda kutafuta fursa zinazoweza kuwanufaisha vijana, akisisitiza kuwa kazi ya maendeleo ya vijana inahitaji hatua za vitendo, ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu kati ya Taasisi za Serikali.

Amesema mafanikio ya mifumo ya vijana hayapaswi kuishia kwenye idadi ya waliowekwa kwenye kanzidata, bali yaonekane katika uwezo wa mifumo hiyo kutatua changamoto, kupunguza urudufu na kuongeza fursa zenye matokeo kwa vijana.

Makamu wa Rais yupo mkoani Rukwa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026.

Habari

Settings