Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Masauni: Rasilimali za bahari zitumike kwa maendeleo yetu

Oct, 08 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema miaka 40 ya Mkataba wa Nairobi ni muda mwafaka wa kuweza kujitathimini kwa namna gani kumeleta tofauti ya Maisha ya watu bila kuathiri mazingira.

Amesema hayo leo Oktoba 8, 2026 wakati akifanya mahojiano maalum na TBC katika kipindi cha ‘Jambo Tanzania’ kuhusu Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12) unaoendelea Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Amesema kama rasilimali za bahari zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja basi maendeleo hayo na mafanikio yaonekane lakini mazingira yanapaswa kuendelezwa na kulindwa kwaajili ya vizazi vijavyo.

“Mkutano huu umeweza kusaidia kuimarisha ushirikiano na kuweka mipango ya pamoja na kuiwezesha kutimiza malengo huku tukishirikisha vijana, wanawake na wafanyabiashara,”

“Mipango ambayo tumeiandaa inahitaji wananchi ambao wataweza kujenga uwezo kwenye masoko na teknolojia na kushirikiana katika kuvutia wawekezaji,” amesema Mhe. Masauni.

Ameongeza kuwa sekta ya Uchumi wa Buluu ni eneo ambalo linategemewa sana katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, hivyo ni eneo ambalo linatazamwa zaidi kwa sasa.

Habari

Settings