Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Masauni aipa NEMC kibarua

Oct, 19 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamadi Masauni, amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya ukaguzi na uhakiki wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira nchini ndani ya kipindi cha wiki mbili ili kubaini kiwango cha uzingatiaji wa sheria hiyo na kuchukua hatua stahiki pale inapohitajika.

Masauni ametoa maelekezo hayo, Oktoba 19, 2026, wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za urejeshaji wa mazingira ya asili katika Mto Mkisi, mkoani Katavi, eneo ambalo hapo awali liliathiriwa na shughuli za uchimbaji wa madini.

Amesisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa mazingira kwa kuweka kipaumbele katika kuzuia uharibifu kabla haujatokea, badala ya kusubiri madhara yatokee ndipo hatua za kurejesha mazingira zichukuliwe.

“Tunapaswa kusimamia ipasavyo utunzaji wa mazingira na kuhakikisha uharibifu unazuiwa mapema, badala ya kusubiri mazingira yaharibiwe ndipo tuanze kuyarejesha,” amesisitiza Masauni.

Amesema ukaguzi huo wa wiki mbili unapaswa kufanyika kwa kina ili kubaini maeneo ambayo sheria za mazingira hazitekelezwi ipasavyo, pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha usimamizi na kuhakikisha hatua zinazostahili zinachukuliwa kwa mujibu wa sheria.

Katika ziara hiyo, Waziri Masauni pia ametembelea mgodi wa Katavi Mining kwa lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utunzaji wa mazingira katika shughuli zote za uzalishaji.

Habari

Settings