Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais ataka uchunguzi wa pembejeo, kwenye zao la korosho

Nov, 12 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesikitishwa na kushuka kwa uzalishaji wa korosho kutoka tani 600,000 hadi tani 400,000 licha ya bei nzuri ya zao hilo, na kumtaka Waziri wa Kilimo kupeleka timu ya watafiti kuchunguza sababu za pembejeo zilizotumika kutotoa matokeo yaliyotarajiwa.

Akizungumza na wananchi wa Mangaka, Wilaya ya Nanyumbu akiwa ziarani mkoani Mtwara, Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kufanyia kazi upatikanaji wa mbolea aina ya salfa ya unga yenye ubora ili kuongeza uzalishaji, baada ya kueleza kuwa salfa ya maji haijaonesha matokeo mazuri.

Amesema kushuka kwa uzalishaji wakati bei ikiwa nzuri kunahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo chake na kuwasaidia wakulima kuongeza mavuno na kunufaika na soko.

Akieleza mipango ya Wizara ya Kilimo, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amesema Serikali itaendeleza dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuinua wananchi kiuchumi kwa kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima.

Amesema wizara itaendelea kuboresha mazingira ya uzalishaji wa korosho na kuhakikisha pembejeo zinafika kwa wakati ili kuwawezesha wakulima kuongeza tija.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amegusia changamoto ya wanyamapori kuvamia makazi ya wananchi na kumtaka Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Chande, kueleza hatua zinazochukuliwa kudhibiti madhara hayo.

Akijibu, Chande amesema wizara imejenga vituo viwili katika maeneo ya Mtamba Swala na Lipika, huku hatua za udhibiti zikihusisha askari 19 na kambi tisa za kukabiliana na wanyama wakali.

Amesema pia Wizara inatumia ndege nyuki mbili kufanya doria pamoja na vizimba vitatu. Aidha, amesema tembo wawili na mamba saba wamevunwa katika juhudi za kupunguza madhara kwa wananchi.

Kuhusu maji, Makamu wa Rais amesema mradi wa Nanyumbu wenye thamani ya Shilingi bilioni 38.4 umeanza kupunguza adha ya wananchi kutafuta maji mbali na makazi yao na kuhatarisha maisha katika Mto Ruvuma.

Amesema amejionea uwekezaji huo wa Serikali baada ya kutembelea na kuweka jiwe la msingi la mradi unaotarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 81,000.

Amewataka wananchi kutunza miundombinu na kuhifadhi chanzo cha maji, huku akisisitiza umuhimu wa umeme wa uhakika katika kuendesha mradi huo, kubangua korosho na kuchakata mazao mengine.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi ametoa rai kwa wananchi kuacha kujichukulia hatua mkononi na kujiingiza migogoro inayoleta madhara. Amesema Jeshi la Polisi litaendelea kuwachukulia hatua wale wote wanaosababisha migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekua ikagharimu maisha ya watu katika maeneo hayo. Amewasihi wakulima na wafugaji kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Habari

Settings