Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais akerwa kasi ndogo ujenzi wa barabara Mbeya

Oct, 16 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Nsalaga (Uyole) hadi Ifisi Jijini Mbeya, licha ya mkandarasi kupata fedha zinazofikia shilingi bilioni 40 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika eneo la Kabwe Jijini Mbeya, baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Makamu wa Rais amesema Serikali haijaridhishwa na kiwango cha kazi kilichotekelezwa, huku wananchi wakiendelea kukabiliwa na kero za vumbi, kufungwa kwa barabara na kukwama kwa shughuli za biashara na usafiri.

Amesema mkandarasi alipokea malipo ya awali ya shilingi bilioni 20 na kuonyesha uwezo wa kupata fedha nyingine bilioni 20 kupitia benki, hivyo matarajio ya Serikali ni kuona maendeleo ya mradi yakiendana na fedha hizo.

Awali, Makamu wa Rais alipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wenye urefu wa kilometa 29, unaogharimu shilingi bilioni 183.708, ambao umefikia asilimia 45.67 ya utekelezaji.

Taarifa hiyo pia ilieleza maendeleo ya miradi mingine mkoani Mbeya, ikiwemo barabara ya Katumba- Lupaso iliyofikia asilimia 6.6, Mbaka - Kibanja asilimia 0.3 na Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani Kasumulu/Songwe kilichofikia asilimia 94.46.

Kutokana na hali hiyo, Makamu wa Rais amemwelekeza Waziri wa Ujenzi kuhakikisha mkandarasi anafungua barabara zilizofungwa kuanzia kesho na kukipa kipaumbele kipande kinachopita katikati ya Jiji la Mbeya, hususan eneo la Mwanjelwa, ili kupunguza adha kwa wananchi na wafanyabiashara.

Aidha, amesisitiza kuwa ujenzi huo ulipaswa kufanyika kwa awamu bila kuathiri shughuli za kiuchumi za wananchi.

Makamu wa Rais amesisitiza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ina mapenzi na wananchi na imewekeza fedha nyingi katika miradi ya maendeleo hivyo watawasimamia watendaji kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa miradi ya maendeleo zinatumika vizuri na kuwanufaisha wananchi na kusisitiza Serikali haitavumilia uzembe.

Amesema Serikali itaendelea kusimamia matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi wa Mbeya na Watanzania kwa ujumla.

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais aliambatana na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe; Waziri wa Ujenzi, Mhe. Masanja Kadogosa; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi; pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba.

Viongozi hao walipata fursa ya kujibu hoja na kero mbalimbali za wananchi wa Mkoa wa Mbeya zilizowasilishwa na wabunge wa mkoa huo, zikiwemo changamoto za upatikanaji wa maji, miundombinu ya barabara, umeme na huduma nyingine za kijamii.

Habari

Settings