Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Kwanza wa Rais ahimiza nchi wanachama COP12 kutekeleza makubaliano

Oct, 09 2026

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amezitaka nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi kuelekeza nguvu katika utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkutano wa 12.

Ametoa wito huo leo Oktoba 09, 2026 wakati akifunga mkutano wa 12 wa Mkataba wa Nairobi (COP12) uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Mhe. Othman alisema ni wakati sasa wa kutekeleza maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo kwa vitendo na kuhakikisha maamuzi yanaleta matokeo.

Alisema kuwa utekelezaji wa maamuzi hayo ni muhimu katika kujenga jamii zenye ustawi na uwezo wa kukabiliana na changamoto za mazingira.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Yussuf Masauni alisema Masauni imepata heshima ya kuandaa COP12 sambamba na kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Mkataba wa Nairobi.

Mkataba huo unalenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira ya bahari na pwani katika Ukanda wa Bahari ya Hindi Magharibi.

Habari

Settings