Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Kwagilwa: Tanzania kinara nchi wanachama COP12

Oct, 16 2026

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa amesema Tanzania inafanya vizuri kati ya nchi wananchama wa Mkataba wa Nairobi wa Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Pwani.

Amesema hatua hiyo ni kutokana na kutungwa kwa kanuni, sera na mikakati katika usimamizi wa bahari na masuala ya hifadhi ya mazingira kwa ujumla ambayo inatekelezwa na kuleta ufanisi na tija kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Mhe. Kwagilwa ametoa kauli hiyo leo Oktoba 16, 2026 katika ofisi za Bunge jijini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira cha kupokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12).

Alisema kuwa jambo ambalo limeisukuma Tanzania kuingia katika mkataba huo ni umuhimu wa kuilinda bahari dhidi ya uchafuzi wa taka ngumu zikiwemo za plastiki, kemekali na maji yanayotiririka kutoka nchi kavu (kwenye viwanda).

Alieleza kuwa kupitia mikataba hiyo ambayo nchi wanachama zimeingia zinaweka mipango ya pamoja ya kuhakikisha bahari inalindwa dhidi ya uchafuzi unaoweza kujitokeza.

“Kama tunavyokumbuka mwaka 2009 tulitunga kanuni ya kudhibiti mifuko ya plastiki yote ilikuwa ni kupunguza uchafuzi wa taka hizo hizo kwani tunatambua kuwa ni dhahiri ikishatoka nchi kavu ni lazima iingie baharini hali inayoweza kusababisha madhara kwa viumbe.

“Pia tuna sheria ya kuzuia utiririshaji wa majitaka ambayo inambana muwekezaji kuyatibu maji yanayotoka kiwandani kabla ya kuyaachi kwani yanayaweza kutiririka hadi baharini,“ alisisitiza Mhe. Kwagilwa.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Prof. Pius Yanda alisema ni muhimu kama nchi iwe na mkakati wa kitaifa utakaoweza kubaini vipaumbele vya kutekeleza.

Alisema lazima kuwepo mpango madhubuti wa kuhamasisha matumizi endelevu ya bahari hususan katika suala zima la kujipatia kipato kutokana na sekta ya uchumi wa buluu ambayo ina viongele mbalimbali.

Pia, Prof. Yanda ambaye pia ni Mbunge wa Buhigwe alishauri kuwepo na mkakati endelevu wa kutafuta fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za uchafuzi wa mazingira hususan ya bahari.

Mkutano wa COP12 ulifanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 6 hadi 9, 2026 na kushirikia nchi wanachama 10 ikiwemo Tanzania, nchi hizo ni Kenya, Comoro, Madagascar, Msumbiji, Shelisheli, Somalia, Afrika Kusini, Ufaransa na Mauritius ambayo imekabidhiwa uenyeji wa COP13 itakayofanyika mwaka 2027.

Habari

Settings