Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

VICE PRESIDENT'S OFFICE

News

Katibu Mkuu Maganga asisitiza weledi kwa watumishi


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga hii leo amekutana na watumishi wa Ofisi yake katika kikao kazi cha kujadili masuala ya kiutendaji na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Pia, Bi. Mary Maganga ametoa rai kwa watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu katika mwaka mpya wa fedha. Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwaasa watumishi kuwa utaratibu wa kufanya tathmini ya utendaji kazi wao wa kila siku na kuweka malengo.

Sambamba na masuala ya kiutendaji, Bi. Mary Maganga pia ametumia fursa hiyo kuwashauri watumishi kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii ambayo kwa namna moja au nyingine yana mchango mkubwa katika ufanishi wa utendaji kazi wa watumishi mahala pa kazi.

Masuala hayo ni pamoja na afya na lishe, kujenga tabia ya kufanya mazoezi, kushiriki shughuli za kijamii na kuendelea kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Afya kujikinga na janga la UVIKO 19.