Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Kamati ya Bunge yataka Jiji la Dar kusimamia vyema dampo Pugu

Oct, 17 2026

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeelekeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuwa na mpango madhubuti wa kusimamia dampo la Pugu Kinyamwezi ipasavyo ili kudhibiti na kukabiliana na athari za afya na mazingira.

Imesisitiza usimamizi wa sheria ya mazingira uwe madhubuti huku ikishauri kupanuliwa kwa wigo wa ujenzi wa madampo ili yajengwe katika maeneo mengine kuzingatia mahitaji hatua itakayosaidia kupunguza changamoto ya kuzagaa ovyo kwa taka.

Maelekezo hayo yametolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Prof. Pius Yanda pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua hali ya mazingira katika eneo hilo mwishoni mwa wiki.

Ziara hiyo imefanyika kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi aliyotoa Septemba 18, 2026 ya kuhusu kuboresha usimamizi wa taka katika dampo hilo.

Aidha, Mhe. Prof. Yanda ambaye pia ni mbunge wa Buhigwe alieleza kuwa wananchi wanaoishi kando ya eneo la dampo ni muhimu afya zao zikapewa umuhimu kwa kuchukua hatua zikiwemo kujenga uzio kulizunguka.

Wakizungumza wakati wa ziara hiyo kwa nyakati tofauti, baadhi ya wabunge walitaka pawepo na ufuatiliaji ili kufahamu ni athari za kiafya kiasi gani zinawaathiri wakazi hao kutokana na moshi, harufu kutokana na mrundiko wa taka kisha kuchukua hatua.

Walisisitiza pawepo na wazabuni wa ukusanyaji wa taka wenye vifaa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa ufanisi ili kuhakikisha miji inakuwa safi na kuvutia hususan Dar es Salaam, jiji ambalo ni kioo cha nchi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa aliyeambatana na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, katika ziara hiyo alisema Serikali itaendelea kuhakikisha suala la uafi wa mazingira linafanyika inavyopaswa.

Alieleza kuwa msimamo wa Serikali ni kuhakikisha na kuhamasisha wadau wanashiriki kikamilifu katika usimamizi wa taka kwa kuzigeuza kuwa fursa hatua itakayosaidia kukabiliana na mrundikano wa taka pasipo sababu.

Halikadhalika, Mhe. Kwagilwa alitaka pawepo na mwekezaji imara wa kusimamia uchakataji wa taka katika Dampo la Pugu kupunguza athari za afya na mazingira kwa jamii inayolizunguka.

Aidha, aliielekeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kushirikiana kwa karibu na taasisi zote zenye mnasaba na mazingira likiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kuhakikisha mradi wa dampo hilo unakuwa endelevu.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imefanya ziara katika eneo la Mto Ng’ombe wilayani Kinondoni na kupongeza jitihada za kuboresha mazingira ya mito mbalimbali mkoani humo.

Akizungumza wakati ziara hiyo Mhe. Prof. Pius Yanda alisema maboresho yaliyofanyika yakiwemo ujenzi wa kingo katika baadhi ya mito yamekuja wakati muafaka ambapo alipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kusimamia ipasavyo mazingira hivyo kujenga ustawi wa afya na hifadhi endelevu ya mazingira.

Halikadhalika Prof. Yanda alisema upo umuhimu wa kuongeza wigo wa upanuzi wa mito mingine ili wananchi wengine wafaidike kwakuwa utunzaji wa mazingira hauna mipaka.

Habari

Settings