Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

VICE PRESIDENT'S OFFICE

News

Waziri Jafo: Wawekezaji muwekeze kwenye maeneo muafaka kuepusha migogoro ya kimazingira


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo ametoa wito kwa wawekezaji nchini kuzingatia maeneo yaliyotengwa kwa shughuli ili kuepusha migogoro ya kimazingira.

Pia ametoa wito kwa wawekezaji kupata cheti kabla ya kujenga kiwanda ili maeneo wanayokusudia kufanya shughuli hiyo yafanyiwe tatmini ya athari kwa mazingira hatua itakayosaidia kuepusha na hasara endapo utajenga kiwanda halafu mradi usitishwe kutokana na changamoto ya kimazingira.

Jafo ametoa kauli hiyo kwenye Mkutano wa Wadau wa Masuala ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM/EIA) uliolenga kupata maoni na ushauri wa namna ya kuboresha mchakato mzima wa kupata vyeti uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema ni kweli Serikali inahitaji watu waje kuwekeza nchini ili kuendeleza sera ya uchumi wa viwanda lakini pamoja na hilo kipaumbele kitakuwa suala zima utuzaji wa mazingira.

Kutokana na hilo waziri huyo alisisitiza kuwa kamwe Serikali kuptia Ofisi ya Makamu wa Rais haitaruhusu shughuli ya uwekezaji inayokwenda kuleta athari za kimazingira kwa wananchi.

“Utakuta mwekezaji ananunua kiwanja katika eneo la makazi ya watu halafu anajenga kiwanda mwisho wa siku anasababisha migogoro hili litakuwa si jema, kwa hiyo niziombe Mamlaka za Serikali za Mitaa ziendelee kutenga maeneo ya uwekezaji ili wawekezaji wajenge viwanda katika maeneo sahihi kuepusha migogoro,” alisisitiza.

Kwa upande mwingine aliwshukuru wadau wanaojitoa katika mazingira na kutoa rai kwao kuwa sehemu ya kutoa elimu kuhusu mchakato huo ili watu wengi waweze kupata uelewa mzuri.

Tukae tuone njia rahiis ya eia kupatikana kwa haraka tuwe na hati ya harsak aanze wakt inakuja eia ili tusimkwamishe

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Mwambe alishauri kuona namna nzuri ya kuwasaidia wawekezaji kwa kurahisha mchakato wa TAM ili kupata wawekezaji wengi hivyo kuongeza wigo wa walipa kodi.

Pia aliwataka wanaofanya tathmini kuwa mabalozi wazuri kuhusu mazingira ya uwekezaji katika nchi yetu ili kuwahamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Aliwataka washirikiane vizuri na wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kuhakikisha michakato yote ya kupata cheti cha athari kwa mazingira inafanyika kwa ufanisi.

Awali akitolea maelezo Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka aliwataka wawekezaji kufuata utaratibu ili kuepukana na changamoto wakati wa mchakato wa kupata cheti.

Akizungumzia mchakato wa kupata cheti mkurugenzi huyo alisema mwekezaji anapaswa kuandaa andiko la TAM sambamba na kuandaa utafiti kuhusu eneo analomiliki ambalo anakusudia kujenga mradi.