Habari
Dkt Muyungi: Hizi ndio fursa za Mkutano wa COP12
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi kutokana na kufanyika kwa Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12) unaoanza leo Oktoba 06, 2026 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na kituo cha runinga cha TBC1, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amesema mkutano huo utawakutanisha washiriki zaidi ya 1460 kutoka nchi 10 wanachama nchi ni
Akizungumzia fursa hizo, Dkt. Muyungi alieleza kuwa asilimia 90 ya bidhaa zinapatikana katika ukanda wa magharibi mwa Bahari ya Hindi ambazo zinakadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani 330 zikihusisha uchumi wa utalii.
Alifafanua kuwa kupitia mkutano huo mkubwa, pamoja na mambo mbalimbali pia kutakuwa na masuala matatu yatakatojadiliwa na washiriki kutokana nchi hizo wananchama.
Dkt. Muyungi alibainisha kuwa kwa mara ya kwanza vijana wataguswa na agenda za mkutano hususan ushiriki wao katika kutambua fursa mbalimbali zinazotokana na bahari.
Alisema kupitia fursa hizo vijana watawezeshwa mbinu mbalimbali za kuchangamkia na kuweza kujipatia kipato hivyo kuchangia pato la mmoja mmoja la nchi.
Halikadhikalika, alieleza kuwa kupitia mkutano huo kundi la wafanyabiashara mbalimbali litakuwa katika nafasi adhimu ya kujifunza na kutambua fursa zinazotokana na sekta ya uchumi wa buluu.
“Wengi tunafahamu kwenye bahari kuna aina mbalimbali za mazao kwa mfano tuna samaki, wavuvi wana nafasi ya kutumia vizuri bahari kuvua samaki kwa ajili ya biashara na kitoweo, pia tunashughuli za utalii zinazotuingizia kipato na pia tunaweza kupata gesia asilia kupitia bahari,” alisema.
Aidha, Dkt. Muyungi aliongeza kuwa kupitia Mkutano wa COP12 wanawake hususan wanaotoka pwani ya Zanzibar wataendelea kunufaika kwa kuwezeshwa na hivyo kupanuka kwa soko la kilimo cha mwani.
Alisema mwani ni mojawapo ya mazao yanayoongeza pato la nchi hivyo wanawake wajasiliamali wanaojihusisha na kilimo hivyo watapata elimu ya kujiendeleza na hivyo kuleta tija.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mojawapo ya nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi mwa Bahari ya Hindi. Nchi hizo ni Kenya,Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini,Visiwa vya Shelisheli, Re- Union(Ufaransa),Comoro , Madagascar na Mauritius.



