Waziri Zungu aipongeza SMZ kwa usimamizi wa mapato

Feb, 14 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa usimamizi wao makini wa kuwaletea maendeleo wananchi wa visiwa hivyo.

Zungu alitoa pongezi hizo jana alipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ Balozi Seif Ali Iddi alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa hivi karibuni.

Alibainisha kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoto hususana za kimazingira lakini Zanzibar imepiga hatua kimaendeleo sambamba na kuongezeka kwa Pato la Taifa.
Aidha, kutokana na changamoto hizo aliahidi kuteua wataalamu maalum wa masuala ya mazingira kwa lengo la kuangalia athari za mazingira zilizojitokeza katika maeneo tofauti.

Waziri huyo aliahidi kupanga ziara maalum ya kuangalia hali ya mazingira katika maeneo ya Zanzibar kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar inayoratibu na kusimamia mambo ya Muungano na Mazingira kwa upande wa Zanzibar.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeweza kunufaisha Zanzibar.

Alisema kuwa zipo fursa zinazowanufaisha wananchi wa Zanzibar ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Bara walioamua kuishi Bara kuendeleza shughuli zao za uwekezji katika kilimo

Settings