Waziri Jafo atoa rai kwa wahitimu kidato cha nne kujiunga vyuo vya ufundi

Jun, 10 2022

Dkt. Jafo amesema hayo tarehe 10 Juni, 2022 jijini Dodoma wakati akifungua Maonesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

Alisema takwimu za mwaka jana zinaeleza kuwa wanafunzi 17,3000 walimaliza kidato cha nne kati yao 90,000 waliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.

“Leo hii kuna vijana wengi wanamaliza kidato cha nne lakini sio wengi wanaoendelea na kidato cha tano na sita vlazima tuboreshe vyuo vyetu vya kati ili vijana ambao watashindwa kuendelea na masomo waende katika vyuo vya kati na ufundi,” alisema Jafo

Alifafanua kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo itatanua wigo wa kuajiri vijana wenye umahiri katika ufundi.

Aliongeza kuwa Tanzania inafanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea na utahitaji vijana ambao wana ujuzi wa kutosha.

“Maeneo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa yanahitaji vijana ambao wamepata elimu ya ujuzi na sasa imeanza mchakato wa kufufua shirika la ndege ambapo hadi sasa kuna ndege 11 na itanunua nyingine hivyo wataitajika vijana wenye ujuzi wa katika uendeshaji na ukarabati wa vifaa hivyo,” alieleza.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda alisema ili kuendelea kukuza bunifu za wanafunzi kutoka vyuo vya ufundi, Serikali imepenga kuanza kuwapatia mikopo ya masomo ili kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivi na hapo itapatikana idadi kubwa ya bunifu itakayoendana na kasi ya mabadiliko yaliyopo kwa sasa katika sekta ya elimu.

Pia Prof. Mkenda aliwataka NACTVET kufanya uchunguzi katika vyuo vyote vya ufundi ikiwa ni pamoja na VETA ili kuhakikisha vijana wanaoandaliwa wanakidhi katika soko la ajira ili kuhakikisha kuwa elimu wanayopewa inakwenda kuwasaidia.

"Niwatake mkafanye case study katika vyuo vyote vya ufundi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapatiwa elimu ambayo itakwenda kuwasaidia katika soko la ajira narudia tena kuwa mkafanye hivyo maana wazazi wanalipa pesa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao ili walete mafanikio katika nchi na familia kwa ujumla," alisema Prof. Mkenda

Pia aliahidi kuwa Serikali itafanya mpango wa maonesho hayo kufanyika na upande wa Zanzibar ili kuendelea kudumisha Muungano. amewataka vijana wanaomaliza elimu ya kidato cha nne na kushindwa kuendelea na kidato cha tano kujiunga na vyuo vya kati na ufundi.


Settings