Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekabidhiwa Tuzo kwa Kujali muda wakati wa utekelezaji wa majukumu leo Februari 21, 2023 ofisini kwake jijini Dodoma.
Amekabidhiwa tuzo hiyo aliyotunukiwa Februari 17, 2023 wakati wa Tamasha la Usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Usiku wa Habari Dodoma Bi.Sakina Abdulmasoud amemkabidhi tuzo hiyo na kumpongeza Mhe. Waziri Jafo.
Bi. Sakina aliyeambatana na Mwanachama wa CPC Bi. Augusta Njoji, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Waziri Jafo wakati wa utekelezaji wa majukumu.