Waziri Jafo ahamasisha upandaji miti Bagamoyo

Oct, 22 2022

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt Selemani Jafo ameshiriki katika zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Shule ya Msingi Mtoni iliyopo katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Akiwa shuleni hapo amepongeza Benki ya Standard Chattered ambao ndiyo waandaaji na wasimamizi wakubwa wa tukio hilo la upandaji miti katika shule hiyo.

Pia, Dkt. Jafo ameziagiza halmashauri zote nchini ambazo hazijafikia malengo ya upandaji miti kama ilivyoeelekezwa na Serikali ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Naagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinafikia malengo ya kupanda miti ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa inayoikabili dunia kwani husababisha, ukame, kuongezeka kwa kina cha bahari na maziwa,"

Naye Mkurugenzi wa Standard Chattered Bw. Herman Kasekende amesema watendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kusimamia zoezi la upandaji miti katika mashule mbalimbali ili kusaidia kutunza mazingira.

Settings