Waziri Bashungwa afungua Warsha ya Maafisa Mazingira

Jun, 03 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema ipo haja ya kuendelea kuwajengea uwezo maafisa mazingira kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Amesema hayo leo Juni 3, 2022 wakati akifungua Warsha ya Maafisa Mazingira wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri zote nchini inayofanyika jijini Dodoma ikiwa ni muendelezo wa Wiki ya Mazingira.

Mhe. Bashungwa alisema wataalamu hao wa mazingira wanapokuwa wanajengewa uwezo wanakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi.

Alisema maafisa hao wanapaswa kuangalia ni namna gani ya kutatua changamoto za kimazingira zinazotokana na masuala ya maendeleo ya miji, viwanda, kilimo pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Nchi hii inahitaji kuendelea, tunahitaji kujenga uchumi, tunahitaji kuongeza tija kwenye kilimo, ufugaji, uzalishaji viwandani, kujenga maghorofa, vyote hivi vinahitaji kwenda sambamba na utunzaji wa mazingira na ninyi ndio wa kutusaidia,” alisisitiza Bashungwa.

Settings