Wataalamu wawezeshaji watakiwa kuboreshaji utekelezaji wa miradi

Jun, 28 2022

Wataalamu Wawezeshaji wa wilaya Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo kame Tanzania (LDFS) wametakiwa kuboresha utekelezaji wa miradi katika wilaya zao.

Wito huo umetolewaleo juni 28, 2022 na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba wakati akifungua Mafunzo ya Tathmini na Ufuatiliaji wa Viashira vya Mradi yanayofanyika mjini Morogoro.

Alisema kumekuwa na changamoto nyingi katika utekelezaji wa miradi zikiwemo kuchelewa hivyo wataalamu hao wanaopatiwa mafunzo wana nafasi ya kwenda kufanya maboresho.

“Wataalamu mnaosaidia katika utekelezaji wa mradi huu, niawaomba sana tunapopata mafunzo haya tukitoka hapa tukaboreshe utekelezaji kwa kubadilisha namna tunavyoihudumia miradi hii katika maeneo yetu,” alisema.

Hata hivyo, Dkt. Komba alisema miradi mingi hususan ya miradi imekwama kwasababu mbalimbali zikiwemo uwezo wa ndani na kukosa uwajibikaji na kujitoa kwa wataalamu katika maeneo husika hivyo ni wakati muafaka kwa washiriki hao wa mafunzo kusimamia kwa ukaribu ili kuleta tija.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa LDFS kitaifa Bw. Joseph Kihaule alisema ni wajibu wa wataalamu wawezeshaji hao kusimamia vyema miundombinu iliyojengwa kupitia mradi ili iwanufaishe.

Alitolea mfano mabwawa na visima na teknolojia za kilimo wazione kama sehemu ya maisha yao kwani viwasaidia katika kuboresha kilimo cha umwagiliaji na hivyo kuongeza usalama wa chakula katika maeneo yao.

Pia Mwezeshaji wa mafunzo Bw. Edson Aspon alisema ni muhimu kufundisha elimu hii kwa wataalamu hao kwa kuwa miradi mingi inayotekelezwa inazalisha gesijoto ambazo athari.

Kutokana na hali hiyo alisema upo umuhimu wa kufanya tathmni ya mchango wa miradi hii katika kupunguza gesi joto inayozalishwa angani hivyo kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mafunzo hayo yametolewa kwa wataalamu waelekezi kutoka halmashauri Kondoa (Dodoma), Mkalama (Singida), Magu (Mwanza), Nzega (Tabora) na Micheweni (Unguja).

Settings