Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais yaendeleza ubabe SHIMIWI

Oct, 03 2022

Timu ya mchezo wa kuvuta Kamba ya Wanawake ya Ofisi ya Makamu wa Rais imeendeleza ushindi katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) 2022 yanayoendelea jijini Tanga.

Katika mchezo wake uliofanyika leo Oktoba 03, 2022 timu hiyo chini ya Kocha Bakari Kibiki imefanikiwa kuifunga timu ya Wizara Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 2-0.

Matokeo hayo yanaipa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais nafasi ya kufanya vizuri zaidi katika michuano hiyo ambayo kwa mwaka huu imetoa wachezaji katika michezo mbalimbali.

Jana Oktoba 02, 2022 timu hiyo ya mchezo wa kuvuta Kamba kwa wanawake ilianza vizuri mashindano hyya SHIMIWI kwa kuifunga 2-0 timu ya Ofisi ya Bunge ushindi uliopokewa vizuri na viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mashindano hayo yanaendelea kufanyika jijini humo kwa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa netiboli, mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake na mpira wa miguu.

Settings