Timu ya IMF yatembelea Tanzania

Feb, 17 2023

Timu ya Shirika la Fedha la Kimataifa ( IMF), yatembelea Tanzania kufanya tathimini ya programu inayofadhiliwa na mkopo nafuu kupitia dirisha la Extended Credit Facility( ECF).

Pamoja na mambo mengine timu hiyo imeangalia maeneo ambayo inaweza kutoa msaada wa kiufundi katika utekelezaji wa mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ndio yenye dhamana ya masuala yote ya Mazingira nchini.Hivyo timu hiyo ilipata fursa ya kukutana na kujadiliana na wataalamu wa Mazingira ili kuona uwezekano wa kutoa msaada wa kiufundi hususan katika masula ya mabadiliko ya tabianchi.

Picha - Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (katikati) akiwa na ujumbe huo ambao umeongozwa na Mshauri Idara ya Afrika, Bw. Charalambos G. Tsangarides (wa pili toka kulia). Bw. Tsangarides amefuatana na Wataalam ikiwa ni pamoja na Mwakilishi Mkazi Tanzania Bw. Jens Reinke ( wa pili toka kushoto).

Settings