Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania, Norway kuimarisha ushirikiano biashara ya kaboni

Jan, 23 2026

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes wakisisitiza ushirikiano zaidi baina ya Tanzania na Norway katika Biashara ya Kaboni.

Viongozi hao wamekutana Jijini Dar es Salaam, Januari 23, 2026 huku wakieleza kuwa Tanzania na Norway wamekuwa marafiki wa muda mrefu ambao wamekuwa wakishirikiana katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo na sasa wataendelea kuimarisha ushirikiano kwenye eneo la Biashara ya Kaboni.

Dkt. Muyungi amesema Tanzania imekuwa ikipiga hatua kubwa kwenye eneo hilo kila siku ambapo Tanzania ndio nchi ya kwanza katika Ukanda wa Afrika Mashariki kuwa na kituo kinachoshughulikia masuala ya Biashara ya Kaboni ambapo kipo mkoani Morogoro.

“Katika kuhakikisha tunazidi kufanya vizuri katika Biashara ya Kaboni tumekua tukizidi kukiboresha kituo chetu kutoka hatua moja kwenda nyingine na siku mbili zilizopita kulifanyika makabidhiano kati ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Ofisi ya Makamu wa Rais,” amesema Dkt. Muyungi.

Kwa upande wake Mhe. Tinnes ameshukuru kwa kusema Tanzania imekuwa ikitoa ushirikiano mzuri hivyo ameshauri kuongeza ushirikiano zaidi kimataifa ili kukabilia na mabadiliko ya tabianchi.

Pia Dkt. Muyungi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Good Neighbors Tanzania Bi. Ilsun Jung pamoja na Mwakilishi Mkazi Shirika la kilimo na Chakula Duniani (FAO) Bi. Tipo Nyabenyi.

Dkt. Muyungi amesema ushirikiano baina ya Tanzania na Korea utaleta manufaa kupitia uzoefu na teknolojia ya Korea katika kukabiliana na changamoto za kimazingira pamoja na kufanikisha lengo la utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa vizazi vya sasa na baadae.

Naye Mwakilishi Mkazi Shirika la kilimo na Chakula Duniani (FAO) Bi. Tipo Nyabenyi ameeleza kuwa shirika hilo litaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kusaidia juhudi za uhifadhi wa mazingira, usimamizi endelevu wa rasilimali za asili, ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuhakikisha usalama wa chakula kupitia mbinu mbadala na sahihi ili kutunza na kuhifadhi mazingira nchini.

Habari

Settings