Habari
Tanzania, Eswatini kuimarisha ushirikiano
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akifanya mazungumzo na Mfalme wa Eswatini, Mswati III kando ya Mkutano wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki, unaofanyika Malabo nchini Guinea ya Ikweta. Tarehe 27 Machi 2026.
Mazungumzo hayo yamelenga namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano, kuchochea maendeleo na mageuzi ya Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) ili kuweza kukabiliana na changamoto na mahitaji ya sasa.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. James Milya, Balozi wa Tanzania Guinea ya Ikweta mwenye makazi yake Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo Mhe. Said Juma Mshana pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Umoja wa Ulaya Mhe. Jestas Nyamanga.



