Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa rai kwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuhakikisha uzalishaji wa mkaa mbadala unaongezeka ili watanzania waweze kuutumia na kusaidia utunzaji mazingira.
Ametoa rai hiyo leo Agosti 12, 2022 wakati wa hafla ya miaka 50 ya STAMICO iliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Jafo alilipongeza shirika hilo na kusema kuwa hatua ya kuanza kuzalisha mkaa mbadala itasaidia katika kupunguza gesi joto duniani.
Pia, alisema kwa sasa utekelezaji wa kuzingatia kila jambo linalofanyika kuendana na sera za mazingira, unafanyika kwa kasi kubwa.