​Sima aagiza kiwanda kuweka mtambo wa kuchakata majitaka

Aug, 04 2020

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mussa Sima amekiagiza kiwanda cha Keds kiwe na mtambo wa kuchakata maji machafu yanayotoka kiwandani hapo kabla ya kuruhusu kwenda kwenye miundombinu.

Sima aliotoa agizo hilo alipofanya ziara katika kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ili kujionea namna wanavyohifadhi mazingira wakati wa uzalishaji wake.

Aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho kutunza mazingira hasa upande wa majitaka na kemikali zote zinazotoka kiwandani na kuhakikisha wana kibali cha kumwaga majitaka kwenye miundombinu iliyojengwa na Serikali.

”Wataalamu kutoka NEMC (Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira) walitoa maelekezo awali waache kumwaga maji machafu yenye kemikali bila kuwepo na utaratibu, sasa wahakikishe wanafuata maelekezo yote waliyopewa na wataalamu hao, natoa miezi mitatu wahakikishe mtambo huo umejengwa,” alisema.

Kwa upande wake Afisa Afya na Usalama wa Keds, Faustine Luhende alisema wa kiwanda kipo kweye mchakato wa kujega mtambo huo na waliomba wapewe miezi miwili kukamilisha wakimshukuru Sima kuwaongezea mwezi mmoja

Aidha naibu waziri huyo alipongeza Kiwanda kinachozalisha nondo cha Lake Steel & Allied Product Ltd kilichopo wilayani humo kwa kuendesha shughuli zake bila kuharibu mazingira.

“Nimefika kiwadani hapa nimejionea namna mnavyotunza mazingira vizuri, nawapongeza kwa hili kwani viwanda vingi vinavyozalisha nondo nchini vimekuwa na changamoto nyingi katika kudhibiti kelele na moshi lakini kweye kiwanda hiki kimeweza kudhibiti chagamoto hizo,”alisema.

Pia akiwa kweye ziara hiyo alikagua Kiwada cha Chisai Innovation Center kinachojishughulisha na uchomaji wa taka hatarishi zinazotoka hospitalini na kushuhudia namna kinavyofanya kazi zake bila kuharibu Mazingira.

Aidha ametoa maelekezo kwa Taasisi husika kusimamia shughuli hizi zinaenda ipasavyo ili kuepuka uchafu wa mazigira na kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi.

Katika ziara hiyo Sima aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Martin Ntemo , Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki, Arnold Mapinduzipamoja na kikosi kazi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani na NEMC.

Settings