Serikali yatekeleza miradi minne ya mazingira

Jun, 05 2023

Serikali imetekeleza miradi minne katika pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya miaka mitano kutoka Mfuko wa nchi zinazoendelea (Least Development Countries Climate Fund-LDCF).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ambapo amebainisha kuwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 19.3 (sawa na shilingi bilioni 46) zimekwishapokelewa.

Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Donge Mhe. Soud Mohammed Jumah aliyetaka kujua kwa miaka mitano iliyopita, Tanzania ilipata kiasi gani cha fedha kutoka katika Mfuko wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (LDCF

Akiendelea kujibu swali hilo Mhe. Khamis alisema Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kutafuta fedha zaidi kutoka kwenye Mfuko wa LDCF ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kadiri fursa zinapopatikana kwa pande mbili za Muungano wetu.

Settings