Serikali yatakiwa kuvibana viwanda visivyofuata taraibu za kimazingira

Sep, 29 2022

Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira imeitaka Serikali kuvichukulia hatua za kisheria viwanda vyote vinavyotekeleza shughuli zake bila kufuata taratibu za kimazingira.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.David Kihenzile amesema hayo baada ya ziara ya kamati hiyo kukitembelea kiwanda kinachozalisha dawa mbalimbali za binadamu cha Shelys Pharmaceutical kilichopo Mwenge mkoani Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo ambayo pia Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ambaye alisema kama Serikali watahakikisha suala la ukaguzi katika maeneo ya viwanda wanalipa umuhimu ili kulinda aina yoyote ya uhalibifu wa mazingira unaoweza kujitokeza.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe.Kihenzile alisema lengo la hatua hiyo ni kulinda afya za wananchi pamoja na viumbe hai. Aidha, alipongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa utunzaji na uhifadhi wa azingira ikiwemo uhifadhi taka na mifumo ya majitaka.

Alisema suala la kutunza mazingira hasa kwa maeneo ya viwanda ni muhimu kwa kuwa litasaidia kulinda afya za wananchi wa maeneo ya karibu badala ya kuwasababishia maradhi.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Viwanda ameitaka Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utengenishaji wa taka ili kutoa urahisi kwa wasafirishaji wa taka hizo kwenda dampo.

Settings