Rais Dkt. Samia: Tumepiga hatua kwa kuzitatua changamoto za Muungano

Jun, 27 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema nchi imepiga hatua kubwa kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto za Muungano 15, hivyo kuongeza imani kwa Serikali.

Mhe. Rais Dkt. Samia amesema hayo wakati wa kuhitimisha Shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bungeni Dodoma tarehe 27 Juni, 2025.

Alisema nchi imepiga hatua kubwa, hususan kwa kuzipatia ufumbuzi jumla ya hoja 15 za Muungano, hatua inayozidi kuongeza imani ya Watanzania kwa Serikali.

Kutokana na hatua hiyo, Mhe. Rais Dkt. Samia aliwaasa Watanzania kuendelea kushikamana na kuwa makini na vitisho vyovyote dhidi ya Muungano huku akiwasihi kuendeleza umoja, utulivu na amani vitu ambavyo ni sifa njema kwa Tanzania.

“Hotuba yangu kwa Bunge nilisisitiza umuhimu wa viongozi wa pande zote mbili za Muungano kukutana na kuzungumzia ustawi wa Muungano wetu. Nafurahi kuwataarifu kwamba maagizo yangu yale yametekelezwa kwa ufanisi zaidi chini
Settings