Ofisi ya Makamu wa Rais yaifunga Bunge mashindano ya SHIMIWI

Oct, 02 2022

Timu ya mchezo wa kuvuta Kamba ya wanawake ya Ofisi ya Makamu wa Rais imeibuka kidedea baada ya kutoka na kuibuka washindi kwa kuwavuta timu ya Ofisi ya Bunge kwa matokeo ya 2-0.

Hayo yamejiri wakati wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) 2022, yaliyofunguliwa leo Oktoba 02, 2022 jijini Tanga.

Mashindano hayo pamoja na mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake yameanza kwa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa netiboli, mchezo wa kuvuta kamba kwa wanaume na wanawake na mpira wa miguu.

Mchezo wa Kamba ndiyo ulikuwa fungua dimba kwa mashindano hayo kwa sharamshamra huku wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakionesha umahiri wao katika mchezo huo chini ya Kocha Bakari Kibiki.

Mashindano ya SHIMIWI yataendelea kesho Oktoba 03, 2022 jijini Tanga ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais inashirikisha timu za wanaume na wanawake katika michezo mbalimbali.

Settings