​Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Mawasiliano zakutana kujadili Kanuni za Taka za Kielekroniki

Jul, 08 2020

Ofisi ya Makamu wa Rais na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Taasisi zake zimefanya Kikao cha pamoja cha kujadili Kanuni za Taka za Kielekroniki leo Julai 8, 2020 jijini Dodoma.

Kikao hicho kimewakutanisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo, Naibu wake Balozi Joseph Sokoine, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Zainab Chaula.

Wajumbe wengine walioshiriki ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka, Mkurugenzi Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira na wajumbe wengine kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, NEMC, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Settings