Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

VICE PRESIDENT'S OFFICE

News

Naibu Waziri Chande: Mabalozi wa mazingira mtusaidie kunusuru vizazi kwa uharibifu wa mazingira


Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Chande ametoa wito kwa mabalozi wa mazingira nchini kuhakikisha wanasaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira ili vizazi vijavyo viweze kukuta nchi ikiwa na mazingira mazuri.

Chande ametoa wito huo Novemba 16, 2021 wakati akifungua Warsha kwa mabalozi hao ikilenga utekelezaji wa Kampeni kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira inayofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa Serikali imewaamini na kuwapa ubalozi ili waisaidie jamii kuweza kuishi kwa amani bila ya taharuki inayosababishwa na uharibifu wa mazingira.

“Tanzania tuna ulazima wa kulinda mazingira, tusifike wakati tukawadhurumu watoto wetu ambao hata hawajazaliwa hii ni dhambi kubwa kwani hata wasomi wanasema mnusuru ndugu yako anayedhurumiwa na anayedhurumu ndio kazi ya mabalozi.

“Niwaombe tutetee vizazi vinavyozaliwa miaka inayokuja wasipate dhuluma ya kuharibiwa mazingira na hivi karibuni tukiwa kwenye ziara mikoani tumeshuhudia karibu asilimi 60 mpaka 70 ya ardhi zimeharibiwa, sasa mabalozi tusaidie hili,” alisisitiza Chande.