Naibu Waziri Chande awataka wananchi kuacha kufanya shughuli kando ya mto

Aug, 22 2021

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande amewataka wananchi wanaojihusisha na shughuli za kibinadamu hususan kilimo karibu na vyanzo vya maji waache mara moja kwani shughuli hizo zinasababisha uharibifu wa mazingira.

Chande alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Misegese Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua athari za uharibifu wa mazingira katika Mto Furuwa.

Alisema kuwa wananchi hao wanapaswa kuzingatia kanuni za kutofanya shughuli zao ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji vya mto huo kwani zinasababisha kingo za mito kubomoka na kusababisha mto kukosa muelekeo na kuleta mafuriko.

Aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama kupitia kwa Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanansimamia kikamilifu kanuni hizo ili wananchi wasifanhye shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji.

Aidha, Naibu Waziri Chande alitoa rai kwa wananchi hao kuwa wavumilvu wakati Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa ushirikiano na Wizara ya Maji, Wizara ya Kilimo pamoja na Mamlaka ya Bonde ikifanya maandalizi ya kutatua changamoto hiyo.

Alielekeza matumizi bora ya ardhi tuwe na matumizi bira tusibiri kusimammiwa tukubali taratibu ili tuhifadhi mto uwe na manufaa

Katika hatua nyingine akiendelea na ziara yake Chande aliagiza mkandarasi wa ujenzi wa daraja eneo la Kiwale akamalihe mradi huo kwa wakati kabla ya Novemba 2021 kwa kuwa unasababisha adha kwa wananchi ikiwemo athari kwa mazingira.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Antipas Mgungusi alisema kuwa mto huo umeleta athari kubwa kwa na kuwa umeharibu miundombinu ya barabara na makazi.

Mbunge Mgungusi aliongeza kuwa wamekuwa wakitumia kiasi kikubw cha fedha katika kudhibiti hali hiyo huku akiomba Serikali ije na suluhu ya kudumu ambayo ni kutibu tatizo hilo kwa kupeleka wataalamu kufanya tathmini ya changamoto hiyo.

Settings