Mwili wa kaka wa Makamu wa Rais waagwa

Jan, 21 2022

Mwili wa Akofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Gerald Mpango ambaye pia ni Kaka wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango umeagwa leo tarehe 21 Januari 2022 katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano Posta Jijini Dar es salaam. Ibada ya kuaga mwili huo imeongozwa na Askofu wa Kanisa la Anglikana dayosisi ya Dar es salaam Jackson Sosthenes.

Akimzungumzia Askofu Gerald Mpango enzi za uhai wake, Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Rukwa Mathayo Kasagala amesema daiama kanisa litakumbuka mchango wa Askofu mpango katika kuliendeleza kanisa ikiwemo kuanzishwa kwa Dayosisi ya ziwa Rukwa.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msaada pamoja na neno la faraja katika kipindi cha msiba huu. Aidha Makamu wa Rais amewashukuru Mawaziri, Viongozi wa Chama pamoja na wote waliojitokeza kawapa faraja familia wakati wote wa msiba.

Makamu wa Rais amemtaja Askofu Mpango kama mtu aliyempenda sana Mungu pamoja na kanisa na alikua hodari wa kuhubiri neno la Mungu. Amesema Askofu mpango alikua msaada na kiongozi katika familia aliyewapenda wanafamilia, kuwalea, kuwashauri na kuwasaidia. Amesema wakati wote aliwasisitiza wanafamilia kusoma na alikua tayari kuwasaidia katika hilo. Aidha amemtaja askofu Mpango kama mtu aliyependa Amani na muda wote alikua msuluhishi wa migogoro ndani na nje ya familia.

Ibada ya kuuaga mwili wa Askofu Gerald Mpango imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali ambao wametoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.

Mwili wa Askofu Mstaafu Gerald Mpango umesafirishwa kuelekea mkoani Kigoma ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 22 Januari 2022 wilayani Kasulu. Mazishi hayo yatatanguliwa na Ibada ya kuaga mwili huo katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea lililopo Kasulu Kigo

Settings