Mhe. Samia ahudhuria kuapishwa Rais Burundi

Jun, 18 2020

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alikuwa miongoni mwa Viongozi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Burundi Evariste Ndayishimiye zilizofanyika jana katika Mji wa Gitega, Uwanja wa Igoma Stadium Nchini Burundi.

Katika sherehe hizo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Akitoa salam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. samia Suluhu Hassan , amempongeza Rais Ndayishimiye kwa ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa hivi karibuni na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Burundi katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Makamu wa Rais Mhe. samia pia aliwapa pole Wananchi wa Burundi kwa kwa msiba mkubwa wa aliyekuwa Rais wa Nchi yao marehemu Pierre Nkurunziza na kuwataka wawe na subira katika kipindi kiki cha maombolezo.

Aidha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiambatana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na NaibuWaziri wa Mambo ya Nje Dkt. walipata nafasi ya kufika nyumbani kwa marehemu Nkurunziza Jijini Bujumbura kwa ajili ya kuitembelea na kuifariji familia akiwemo mjane na watoto wa marehemu, ambapo amemuomba Mwenyezi Mungu kuwapa uvumilivu na kuwa na subira katika kipindi hiki cha maombolezo.

Katika sherehe hizo za kuapishwa Rais mpya wa Burundi pia zilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amerejea Nchini akitokea Nchini Burundi jana Usiku.

Settings