Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Masauni: Serikali yaimarisha usimamizi wa rasilimali

Aug, 12 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Serikali inaendelea kuimarisha usimamizi endelevu wa ardhi na rasilimali za asili ili kupunguza uharibifu wa ardhi katika kukabiliana na athari za kuenea kwa hali ya jangwa na ukame.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma Agosti 12, 2026 wakati akiwasilisha taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Kuhusu Programu ya Kitaifa ya Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame (2025 – 2030).

Mhe Masauni amesema lengo ni kupunguza uharibifu wa ardhi na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kupitia uhifadhi na urejeshaji wa afya ya ardhi, kupunguza umaskini na kuimarisha usalama wa chakula kwa kuboresha matumizi ya rasilimali na kuongeza kipato.”

“Lengo lingine ni kuimarisha uwezo wa kukabiliana na hali ya jangwa na ukame kwa kuboresha usimamizi wa rasilimali za maji na mifumo ya tahadhari, Kukuza usimamizi endelevu wa rasilimali za asili, ikiwemo ardhi, misitu, maji na nyanda za malisho,” amesema Mhe, Masauni.

Amesema Serikali inaendelea na kampeni za uhamasishaji kote nchini kupitia vyombo vya habari, programu za mafunzo, ili kuelimisha jamii na wadau kuhusu umuhimu wa kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na ushirikishwaji wa wadau.

“Serikali inaendelea kushirikisha wadau wakiwemo asasi za kiraia na sekta binafsi katika upangaji na utekelezaji wa mipango ya kupambana na kuenea kwa jangwa na ukame.”

Pia kuimarisha Ufutiliaji wa takwimu na taarifa, Serikali inakamilisha mfumo wa kidijitali (e-Mazingira) ambao utawezesha upatikanaji wa taarifa na takwimu za hali ya mazingira ambazo zitawezesha kufuatilia athari za kuenea kwa hali ya jangwa na ukame.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) ni nchi mwanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame (UNCCD), Mkataba huu ni kati ya Mikataba mitatu iliyopitishwa kwenye mkutano wa Mazingira na Maendeleo (UNCED) uliofanyika nchini Brazil mwaka 1992.

Tanzania ilijiunga na Mkataba huu mwaka 1992 na ulianza kutekelezwa Aprili, 1994 na JMT iliridhia Mkataba huu Juni 29, 1997 na hadi sasa nchi wanachama Duniani wapo 197 huku Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwa Kiungo kati ya Serikali ya JMT na Sekretarieti ya Mkataba.

Habari

Settings