Makamu wa Rais azindua kampeni ya upandaji miti kwenye vyanzo vya maji

Nov, 16 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 16 Novemba 2022 amezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji, zoezi lililofanyika katika chanzo cha maji cha Nzovwe 1 kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi wote wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanafanya jitihada za ziada katika kulinda vyanzo vya maji pamoja na kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kuondoa wananchi walioweka makazi katika vyanzo vya maji na kuharibu vyanzo hivyo.

Pia Makamu wa Rais amesema umefika wakati Wizara ya Ardhi kufanya upimaji wa ardhi kwaajili ya maeneo mahususi ya ufugaji na kuondokana na ufugaji holela wa mifugo unaochangia uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais amewaasa Wakulima, Wafugaji na wenye Viwanda kutambua suala la matumizi ya rasilimali maji linapaswa kuwa endelevu kwa kutochafua na kuharibu vyanzo vya maji.

Amewataka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuongeza juhudi katika kila mkoa kutambua miti rafiki wa maji na kuwa na miche ya kutosha itakayopandwa katika vyanzo vya maji. Aidha amewaagiza kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya miti rafiki ya maji na kuondokana na makosa yaliofanyika katika baadhi ya maeneo na kukausha vyanzo vya maji.

Makamu wa Rais ameagiza Wakuu wa Mikoa wote nchini kuzindua rasmi kampeni ya upandaji miti rafiki wa maji katika maeneo yao ili kufikia lengo la kupanda miti milioni 2.5 lililowekwa mwaka huu.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amefungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde unaofanyika Jijini Mbeya tarehe 16- 18 Novemba 2022.

Akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Makamu wa Rais amesisitiza ushirikiano wa taasisi zote za Serikali, Chama, wadau wote ikiwemo machifu waliopo mikoani na viongozi wa dini kuwa ndiyo njia bora zaidi katika kusimamia rasilimali za maji hapa nchini na zitakazosaidia kukabiliana kirahisi na uharibifu wa mazingira.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 16 Novemba 2022 amezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upandaji miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji, zoezi lililofanyika katika chanzo cha maji cha Nzovwe 1 kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi wote wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanafanya jitihada za ziada katika kulinda vyanzo vya maji pamoja na kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kuondoa wananchi walioweka makazi katika vyanzo vya maji na kuharibu vyanzo hivyo.

Pia Makamu wa Rais amesema umefika wakati Wizara ya Ardhi kufanya upimaji wa ardhi kwaajili ya maeneo mahususi ya ufugaji na kuondokana na ufugaji holela wa mifugo unaochangia uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais amewaasa Wakulima, Wafugaji na wenye Viwanda kutambua suala la matumizi ya rasilimali maji linapaswa kuwa endelevu kwa kutochafua na kuharibu vyanzo vya maji.

Amewataka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuongeza juhudi katika kila mkoa kutambua miti rafiki wa maji na kuwa na miche ya kutosha itakayopandwa katika vyanzo vya maji. Aidha amewaagiza kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya miti rafiki ya maji na kuondokana na makosa yaliofanyika katika baadhi ya maeneo na kukausha vyanzo vya maji.

Makamu wa Rais ameagiza Wakuu wa Mikoa wote nchini kuzindua rasmi kampeni ya upandaji miti rafiki wa maji katika maeneo yao ili kufikia lengo la kupanda miti milioni 2.5 lililowekwa mwaka huu.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amefungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde unaofanyika Jijini Mbeya tarehe 16- 18 Novemba 2022.

Akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Makamu wa Rais amesisitiza ushirikiano wa taasisi zote za Serikali, Chama, wadau wote ikiwemo machifu waliopo mikoani na viongozi wa dini kuwa ndiyo njia bora zaidi katika kusimamia rasilimali za maji hapa nchini na zitakazosaidia kukabiliana kirahisi na uharibifu wa mazingira.

Settings