Makamu wa Rais ashiriki ufunguzi wa Mkutano wa Jumuiya ya Madola

Jun, 24 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 24 Juni 2022 ameshiriki ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Wakuu wa Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya za Madola (CHOGMU 2022) unaoendelea Kigali nchini Rwanda. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili tarehe 24-25 Juni 2022.

Pia mkutano huo umetanguliwa na mikutano mbalimbali iliojikita katika vipaumbele vya kisera kama vile utawala bora, utawala wa sheria na Haki za Binadamu,Vijana, Afya , teknolojia na uvumbuzi,Maendeleo endelevu katika Biashara na Uchumi pamoja na kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi na utunzanji mazingira.

Akihutubia mkutano huo Rais wa Rwanda mheshimiwa Paul Kagame amesema jumuiya ya madola inapaswa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza duniani na sio kuchagua maeneo ya kutatua changamoto hizo. Aidha ameongeza kwamba nchi wanachama wa Jumuiya za Madola hazinabudi kutambulika kwa utawala bora na utawala wa sheria pamoja na ulinzi wa haki. Aidha ameongeza kwamba Jumuiya ya Madola inapswa kuwa tayari kupokea mapendekezo mapya pamoja na wanachama wapya na kutumia njia ya mazungumzo katika kutatua migogoro itakayojitokeza ndani ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola mheshimiwa Patricia Scotland amesema mkutano huo ni fursa kwa mataifa kuunganisha mawazo na kutoa ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili dunia hususani za kiuchumi zilizosababishwa na Uviko 19, mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na migogoro ya kimataifa iliopelekea kupanda kwa gharama za chakula na nishati ya mafuta duniani.

Amesema nchi wanachama zinapaswa kuaminiana na kusikilizana kwa manufaa ya wananchi bilioni 2.5 waliopo katika nchi za Jumuiya ya Madola.

Settings