Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameshiriki katika ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino katika sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Ikulu hiyo Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei 2023.
Ufunguzi huo umeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Bunge, Mahakama, Dini, Vyama vya Siasa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Machifu, Viongozi Wastaafu, Wasanii, na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Nchi.