Makamu wa Rais aipongeza Tume ya Haki za Binadamu

Aug, 30 2020

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora kwa kazi nzuri inayofanywa na Tume hiyo kwa kutatuwa changamoto mbalimbali za wananchi na kuweza kupata haki zao pale wanapodhurumiwa.

Samia alisema hayo alipokutana na Ujumbe wa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora uliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu walipomtembelea kwenye Makazi yake Kilimani Jijini Dodoma.

Aidha Makamu wa Rais aliipongeza Tume hiyo kwa kuweza kubadilika na kufanya kazi vizuri pamoja na kutenda haki kwa wananchi na taasisi zote kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Msaafu Mathew Mwaimu aliipongeza Serikali kwa kuwaletea wananchi maendeleo na kuitakia kila la heri katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Hata hivyo, Jaji Mwaimu alisema kuwa Tume yake haipendezewi na vitendo vya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ambao wamekuwa wakisema watu baada ya kunadi sera za vyama vyao.

Settings