Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ahamasisha jamii kuhifadhi mazingira

Jun, 15 2023

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Bw. Abdalla Shaibu Kaim ameihamasisha jamii kuendelea kulinda na kuhifadhi mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Bw. Kaim ametoa kauli hiyo wakati Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika mbio hizo kiongozi huyo pia ametumia nafasi ya kupanda mti katika bwawa la kuhifadhi maji Mabayani lililopo eneo la Pande wilayani humo pamoja na kukagua vyanzo vya maji.

Wakati huo Bw. Kaim ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TANGA UWASA)kwa kushiriki katika utunzaji wa vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira.


Mwenge wa Uhuru unaendelea kukimbizwa katika mikoa mbalimbali nchini na kwa mwaka 2023 unachagizwa na kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.

Kutokana na umuhimu wake zoezi la utoaji wa elimu ya uhifadhi wa mazingira inaendelea kutolewa kwa wananchi wanaojitokeza katika maeneo mbalimbali Mwenge wa Uhuru unakopita.

Settings