Kamati ya Bunge yatembelea Mradi wa mazingira wa LDFS Kondoa

Mar, 12 2022

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira wametembelea na kukagua Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame Tanzania (LDFS) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo Machi 12, 2022

Wakiwa katika ziara hiyo wametembelea shughuli ya utengaji wa msitu wa Intela wenye ukubwa wa hekta 863.4 kuwa hifadhi ya kijiji cha Haubi pamoja na kukagua shughuli za kilimo msitu ya alizeti katika shamba darasa lililopo Kijiji cha Haubi.

Pamoja na Kondoa pia mradi wa LDFS unatekelezwa katika wilaya za Mkalama (Singida), Magu (Mwanza), Nzega (Tabora) na Micheweni (Zanzibar).

Malengo ya mradi ni kuboresha usimamizi endelevu wa ardhi na kuwezesha urejeshwaji wa mifumo ikolojia iliyoharibika inayochangia kutoa huduma muhimu za uzalishaji kwenye maeneo ya ardhi, maji, misitu na bionuai kwa madhumuni ya kuongeza uzalishaji wa chakula.

Settings