Kamati ya Bunge yapongeza kiwanda kwa kufuata sheria za mazingira

Sep, 27 2022

Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira imeupingeza uongozi wa kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited cha uzalishaji wa nyaya za umeme kwa kufuata sheria na taratibu za utunzaji wa mazingira.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe.David Kihenzile katika ziara ya kamati hiyo kwenye kiwanda hicho kilichopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Amesema wameridhishwa na kiwanda hicho kwani hakitoi gesi chafu, majitaka au taka ngumu ambazo zinaweza kuwa kero na kuathiri afya ya wananchi ambao wanaishi karibu na kiwanda hichio.

Mwenyekiti huyto alisema kamati imeridhishwa na mpango wa uhifadhi wa mazingira kwenye kiwanda hiki na tunawasihi viongozi na wafanyakazi wa kiwanda kuendelea kufanya vizuri katika utunzaji wa mazingira kwenye eneo hili la kiwanda.

Pia, ametoa wito kwa viwanda vingine viendelee kufanya vizuri katika suala la uhifadhi wa mazingira ili kuepukana na mlipuko wa magonjwa hatarishi yatokanayo na uchafuzi wa mazingira kwenye viwanda vyetu.

Pamoja na hayo Mhe.Kihenzile amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kuhakikisha viwanda vinavyozalisha bidhaa nchini vinafuata sheria, taratibu na kanuni za uhifadhi wa mazingira.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamisi Hamza Khamisi amesema hawajapata taarifa ya malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu kero za kiwanda hicho hivyo amewapongeza kwa kuzingatia uhifaddhi na utunzaji wa mazingira kwenye eneo hilo.

Hata hivyo, ametoa maelekezo kwa uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanatoa msaada kwa wananchi ambao wanaishi karibu na kiwanda hicho kwa kujenga miradi mingine mikubwa ikiwemo miradi ya maji, elimu, afya na miradi mingine mingi.

Naye kurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira (NEMC, Mhandisi Redempta Samweli amesema watahakikisha wanasimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu kuboresha utunzaji wa mazingira kwenye kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited.

Settings