Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt. Muyungi, Dkt. Liwenga wateta ushirikiano usimamizi Ziwa Tanganyika

Feb, 24 2026

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika, Dkt. Emma Liwenga.

Mazungumzo hayo yalifanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, leo Jumanne Februari 24, 2026, ambapo Dkt. Muyungi amempongeza Dkt. Liwenga kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo ambayo ni muhimu kwa mustakabali endelevu katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira ya ziwa hilo.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Muyungi ameeleza umuhimu wa ushirikiano baina ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Mamlaka hiyo katika kuimarisha utekelezaji wa Mkataba wa Usimamizi wa ziwa hilo la pili kwa ukubwa wa kina duniani likiwa na utajiri mkubwa wa bayoanuai.

Kwa upande wake, Dkt. Liwenga alimshukuru Dkt. Muyungi kwa maelekezo aliyompatia wakati wa kikao hicho na kuahidi kushirikiano na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili ya mustakabali endelevu wa rasilimali zilizopo katika ziwa hilo.

Mkataba wa usimamizi wa Ziwa Tanganyika unalenga kuimarisha uhifadhi wa mazingira na usimamizi endelevu wa rasilimali zilizopo katika bonde la ziwa hilo, ikiwemo samaki, maji na bioanuwai.

Tanzania ni Nchi mwanachama wa mkataba wa usimamizi endelevu wa Ziwa Tanganyika, inashirikiana na nchi nyingine wanachama ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na Zambia kwa ajili ya usimamizi na uendelezaji wa ziwa hilo.

Awali kabla ya uteuzi wa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika, Dkt. Liwenga alikuwa Mshauri wa masuala ya Mazingira wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Habari

Settings