Dkt. Mpango kumwakilisha Rais Samia Jukwaa la Uwekezaji

Oct, 31 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 31 Oktoba 2022 amewasili Abidjan nchini Ivory Coast ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Uwekezaji Barani Afrika litakalofanyika tarehe 02-04 Novemba 2022.

Makamu wa Rais anatarajia kuongoza mazungumzo baina ya Tanzania na wawekezaji mbalimbali kuhusu uwekezaji katika miradi ya kimkakati nchini Tanzania katika sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji, Usafirishaji na Uchukuzi.

Jukwaa la Uwekezaji Barani Afrika linaratibiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na waanzilishi wa Jukwaa hilo na linalenga kuwakutanisha Wawekezaji, Sekta Binafsi na Sekta ya Umma ili kuweka mikakati ya kufadhili miradi endelevu.

Jukwaa hilo linashirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa pamoja na wafanyabiashara.

Settings