Dkt. Jafo atoa maelekezo soko la machinga Dodoma

Jul, 26 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo Dk.Jafo amemuaelekeza mkandarasi anayejenga mradi wa soko la machinga jijini Dodoma kuimarisha mfumo wa maji safi na majitaka ili kulinda mazingira.

Ametoa maelekezo hayo Julai 26, 2022 alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua mifumo ya utunzaji mazingira sokoni hapo na kubainisha kuwa ni maji mengi yatakuwa yanazalishwa wakati wa uendeshaji wa soko hilo na kuwa bila mifumo imara kutachangiwa uchafuzi wa mazingira.

Aidha, Dkt. Jafo ameuagiza Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kufunga mifumo ya gesi asilia katika soko hilo ili kuzuia uchafuzi wa mazingira wakati soko hilo likianza kutumika na kusababisha wafanyabiashara wa upishi kutumia nishati isiyo rafiki kwa mazingira.

Alimtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kusimamia suala la uwekaji wa mfumo mmoja wa gesi asilia utakaowasaidia watumiaji kulipa ankara (bili) kuliko kila mmoja kuweka mtungi wake.

Pia waziri huyo alisema soko hilo ni lazima liwe na mtu wa kusimamia shughuli za usafi wa mazingira kwa kulifanya liwe na muonekano mzuri huku akimpongeza mkandarasi kwa kufanya kazi nzuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usimamizi wa Taka ngumu Bw. Dickson Kimaro aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Jiji aliahidi kuyafanyia kazi maagizo ya Waziri Jafo.

Settings