Wasifu

Mhe.Samia Suluhu Hassan
Mhe. Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais, 2015 - 2021

Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye kwa sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alizaliwa mjini Zanzibar Januari 27,1960.

Elimu yake

Mhe. Samia Suluhu Hassan alipata elimu ya Msingi katika shule mbalimbali ikiwemo Chwaka iliyoko Unguja mwaka 1966 hadi 1968, Shule ya Msingi Ziwani iliyoko Pemba kuanzia mwaka 1970 hadi 1971 na shule Msingi Mahonda iliyoko Unguja mwaka 1972. Mwaka 1973 mpaka 1975, Mhe. Samia alijiunga na masomo ya Sekondari katika shule ya Sekondari Ngambo na Lumumba.

Mwaka 1977 Mhe. Samia alijiunga na Taasisi ya Fedha na Utawala Zanzibar (ZIFA) ambako alitunukiwa Cheti cha Takwimu na baadaye aliajiriwa na Wizara Mipango na Maendeleo. Baadaye alijiunga na Taasisi ya Maendeleo na Utawala Mzumbe (IDM) ambayo sasa ni Chuo Kikuu Mzumbe mkoani Morogoro kwa masomo ya Stashahada ya Utawala (Public Administration).

Mwaka 1989 Mhe. Samia alijiunga na Chuo cha Taifa cha Usimamizi na Utawala wa Ummaki kilichoko Lahore nchini Pakstan kwa ajili ya masomo ya Utawala na baadaye mwaka 1991 aliendelea na masomo ya Utawala kwa Viongozi katika Chuo cha Hyaerabad nchini India. Baada ya mafunzo hayo mwaka 1992 aliajiriwa kwenye Mradi uliokuwa ukifadhiriwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Mhe. Samia alijiendeleza kimasomo kwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza kwa masomo ya Elimu ya juu ya Uchumi ambako alihitimu Stashahada ya juu ya Uchumi. Mwaka 2004 aliendelea na masomo ya Shahada ya Umahiri ya Maendeleo ya Uchumi kupitia Programu shirikishi iliyokishirikisha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Chuo Kikuu cha Southern New Hampshire cha nchini Marekani.

Uzoefu wa Kisiasa

Mwaka 2000 Mhe. Samia aliteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kuwa Mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi kupitia Viti Maalum ambapo pia aliteuliwa na Rais wa Zanzibar wa wakati huo Mhe. Amani Karume katika nafasi ya Uwaziri na kuwa miongoni mwa wanawake walioshika wadhifa wa juu katika Baraza la Mawaziri. Mwaka 2005 aliteuliwa tena na kuendelea na nafasi ya Uwakilishi katika Baraza hadi mwaka 2010 ambapo aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Makunduchi na kufanikiwa kushinda kwa asilimia 80.

Kufuatia mafanikio ya kisiasa aliyoyapata ya kuwa mmoja wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitokea Zanzibar, akiwa katika nafasi hiyo aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano. Mwaka 2014 Mhe. Samia akiwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo ambalo lilikua na jukumu la Kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya.Pia Julai 2015, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa Chama hicho Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alimteua kuwa mgombea mwenza katika nafasi ya Makamu wa Rais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Settings
VPO | Wasifu