Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu Nishati Safi ya Kupikia pamoja na Ujumbe kutoka Saudi Arabia
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Februari 19,2025 jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo uliambatana na Balozi wa Ufalme wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya bin Ahmed Okeish, Meneja wa Mpango wa Nishati Safi ya Kupikia Bi. Reema Al Ashgar na Mhandisi wa mradi Bw. Faisal Al Mahsn wote kutoka Wizara ya Nishati ya Saudia.
Waziri Masauni amesema ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia baada ya Jumuiya za Kimataifa kuanzisha kampeni hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa wa kwanza kuibeba na kuileta nchini Tanzania kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo, jambo ambalo limeongeza msukumo na kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia hasa katika maeneo ya vijijini.
“Ofisi ya Makamu wa Rais ina dhamana ya Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira, hivyo agenda ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ni eneo muhimu sana hili katika kutunza mazingira.