Waziri Jafo: Sijaridhishwa mwenendo ujenzi wa jengo la Ofisi

Feb, 27 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameonesha kutoridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.

Kutokana na hali hiyo amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais kumuandikia barua Mkandarasi Kampuni ya SUMA JKT ya kuonesha kutoridhishwa na utendaji wao wa kazi hiyo ya ujenzi.

Dkt. Jafo ambaye aliambatana na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Muungano Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Menejimenti ya Ofisi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, amechukua hatua hiyo baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa jengo hilo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba jijini hapa leo Februari 27, 2023.

Amesema kuwa Serikali haitakubali kuona mkandarasi huyo anashindwa kukamilisha kazi ya ujenzi wa jengo hilo kwa wakati ambapo kwa mujibu wa mkataba inatakiwa iwe imekamilika ifikapo Novemba 2023.

Pamoja na hayo pia, Waziri Jafo amesisitiza baadhi ya kazi zinazokwenda sambamba ziendelee kufanyika ili kuokoa muda wa ukamilishaji wa ujenzi wa jengo hilo.

“Naomba niwaambie SUMA JKT ninyi ni taasisi ya Serikali lakini mnatucheleweshea kazi nadhani sasa tuangalie kama kuna baadhi ya vifaa vya ujenzi tukubaliane na mkandarasi na msimamizi elekezi Serikali tuvinunue maana inawezekana mnatuambia vifaa vipo stoo kumbe havipo, hatutakubali, maana kazi hii ilipaswa kuisha mwezi wa kumi na moja mwaka huu sasa kwa mwenendo huu tutajikuta unafika Januari, haiwezekani,“ alisem.

Februari mosi, 2023 Waziri Jafo alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo na kutoa wiki mbili kwa mkandarasi huyo pamoja Msimamizi Elekezi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha wanakamilisha kazi ya kupiga lipu (plasta) kuta zote.

Dkt. Jafo katika ziara hiyo alisema kuwa anashangazwa na namna ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais unavyosuasua tofauti na majengo mengine ambayo yako katika hatua nzuri.

Ofisi ya Makamu wa Rais ilisaini mkataba wa sh. bilioni 18.8 na Kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT Oktoba 13, 2021 na kutakiwa kukamilisha kazi hiyo Novemba 09, 2023 kutakiwa kukamilisha ujenzi huo uwe wa haraka kwa kuzingatia ubora, viwango na kasi.

Tulitoa nikut plasta ikamilke ukiangalie kuta bado kazi bado haijaisha menejimeti haiko viziri kuna kazi zinawez kufanyika kwa wakati mmoja hazifanyika

Settings