Waziri Jafo awapa kongole NEMC kwa kusimamia Sheria ya Mazingira

Sep, 25 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa usimamizi na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira kwa ustawi wa kizazi cha sasa na cha badae.

Amezitoa pongezi hizo leo Septemba 25, 2023 alipotembelea banda la NEMC wakati wa Maonesho ya sita Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya Bombambili (EPZA) mjini Geita.

"Niwapongeze sana kwa sababu mmekuwa msaada mkubwa sana katika Ofisi yangu hususani katika suala la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mazingira," amesema Dkt. Jafo.

Aidha, Waziri Jafo amelisisitiza Baraza hilo kutumia fursa ya maonesho ya madini kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira yakiwemo madhara yanayoweza kutokea pindi mazingira yakiharibika.

Sanjari na hilo pia, amesema ni muhimu kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu wanaotumia zebaki kuchenjulia kupewa elimu kuhusu madhara ya matumizi ya kemikali hiyo.

Settings