Vijana wadakiwa kuchangamkia Fursa Biashara ya Kaboni

Oct, 13 2023

Biashara ya Kaboni nchini imezidi kushamili kutokana na jamii kuhamasika katika kutunza misitu baada ya kuona wenzao wakinufaika na biashara hiyo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis akiongea na vijana zaidi ya 300 waliojitokeza katika mdahalo wa masuala ya mazingira uliofanyika leo Oktoba 13, 2023 Babati, mkoani Manyara ambapo mada ilikuwa ikisema ‘Nafasi ya vijana katika utunzaji wa mazingira’ amewaambia vijana wachangamkie biashara ya Kaboni.

Amesema biashara ya kaboni inaingiza fedha nyingi sana, vijana wachangamkie fursa hiyo, hivyo wapate elimu sahihi ili kujua ni namna gani biashara hiyo inafanyika na inakuwaje.

“Biashara hiyo unaweza usiielewe usipopata elimu husika. Hiyo ni biashara inayoingiza fedha nyingi za kigeni. Napenda kuwaambia kwamba serikali ipo tayari kuwaelimisha na kuwahamasisha vijana.”

Amesema elimu ya kisayansi kuhusu biashara ya kaboni inatolewa katika kituo cha ‘Carbon Monitoring Centre’ ambacho kipo Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.

Pia, aliwakumbusha vijana kutunza amani ya taifa akieleza mataifa mengi amani inaharibika chanzo inakuwa ni vijana, hivyo hata kuitunza amani ya taifa vijana ndio wanaowajibu mkubwa wa kusimamia hilo.

“Amani ya Nchi yetu ya Tanzania ipo kwa wananchi lakini kubwa ni vijana, jambo la kuenzi kiongozi, kuhakikisha afya njema halitokuwa kama hakutakuwa na amani ya kutosha, hivyo tusipoituza nchi yetu hawezi kutoka mtu nje akaja kuitunza na kuendelea amani yetu.”

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2023, idadi ya vijana inakadiriwa kufika milioni 20 ambao ndio nguvu kazi ya taifa katika kuleta maendeleo.

Settings